Kivuko chauwa watu 10 Misri

WATU 10 kati ya 15 wamekufa baada ya kivuko walichokuwa wamepanda kuzaka katika Mto Nile nje kidogo ya mji mkuu wa Misri, mamlaka inaeleza.

Watano walionusurika waliwahishwa hospitalini na baadaye kuruhusiwa, Wizara ya Wafanyakazi ilisema katika taarifa.

Wizara ilitenga fidia ya pauni 200,000 za Misri kwa kila familia ya marehemu na pauni 20,000 kwa kila mmoja wa watano waliojeruhiwa.

Advertisement

Tukio hilo lilitokea katika mji wa Monshat el-Kanater huko Giza, ambao ni moja ya majimbo matatu yanayounda Greater Cairo.

Wamisri wengi hufanya safari zao kwa kutumia boti kila siku, haswa katika Upper Egypt na Delta ya Nile.