Kivuko kikamboni kuendeshwa na sekta binafsi – Samia

SERIKALI imesema itaingia mkataba na sekta binafsi kwa ajili ya uendeshaji wa kivuko cha Kigamboni lengo ikiwa ni kuongeza ufanisi na kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi, Rais Samia Suluhu Hassan amethibitisha leo akiwa Kigamboni, mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji Kigamboni, Rais Samia amesema kwa sasa kuna kivuko kidogo cha mtu binafsi kinachosaidia kutoa huduma kati ya Dar es Salaam na Kigamboni baada ya vivuko vikubwa kupata hitirafu.

“Tunatambua kuna kivuko kinafanyiwa matengenezo. Vilevile kuna kivuko kipya kinajengwa na kitakapofika tutaingia mkataba na sekta binafsi ili kukuindesha,” amesema Rais Samia.

Wakazi wa Kigamboni wamekuwa wakilalamikia huduma duni za kivuko kutokana na changamoto za matengenezo ya mara kwa mara na wakati mwingine huduma mbovu. Mbunge wa Kigambani Dk. Faustine Ndugulile amemwambia Rais Samia wananchi wa Kigamboni baado wanateseka na dosari za kila siku za uendeshaji wa kivuko hicho.

“Tunaomba kama inawezekana kivuko hicho kikabodhiwe kwa sekta binafsi,” alishauri Dk Ndugulile.

Rais Samia amekiri kuwa uendeshaji wa kivuko hicho ni mzigo kwa serikali na kwamba kivuko hicho kikiwa chini ya usimamizi wa sekta binafsi kitapunguza mzigo kwa serikali.

Habari Zifananazo

Back to top button