Kivumbi uchaguzi Chama cha Wafugaji

DODOMA: TUME ya Uchaguzi ya Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT) imewataka wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ngazi ya Taifa ndani ya chama hicho kufanya kampeni zenye staha ambazo hazitaleta vurugu wala kuwagawa wafugaji nchini

Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Chama hicho, Charles Malangwa wakati akitoa taarifa Kuhusu mwenendo wa uchukuaji fomu na urejeshaji kuelekea uchaguzi wa Aprili 8, Mwaka huu.

“Huko wanakojinadi ni vyema wakazingatia maadili ya chama chetu, watengeneze kampeni za kistaarabu, wajenge wanachama wetu kwa sababu watakapoendesha kampeni zenye mwelekeo mbaya watawagawa wanachama hawa mwisho wanakuja kuwaongoza haohao” Charles Malangwa

Mlezi wa chama hicho, Joseph Makongoro ametoa nasaha kwa wagombea na na viongozi wa Tume ya uchaguzi kuhakikisha wanaendesha uchaguzi wa huru na haki bila kuvunja katiba ya Chama Hicho

Hata hivyo Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Tanzania CCWT, Mrida Mshota, ambaye ni miongoni mwa wagombea na nafasi hiyo ameeleza baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja tangu ashike kijiti cha uongozi

“Wafugaji wapatao 8413 wameanza kupatiwa mikopo kutoka kwenye mabenki mbalimbali na kutuwezesha Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuuza mazao yatokanayo na mifugo nje ya Nchi yenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 50, kwa mana hiyo kazi iliyofanyika ni kubwa” alisema Mrida Mshota.

Chama cha wafugaji Tanzania kinatarajia kufanya Uchaguzi mkuu Aprili 8, Mwaka huu Jijini Dodoma

Habari Zifananazo

Back to top button