Kiwanda cha kisasa mazao ya mifugo kujengwa Z’bar

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), inatarajia kujenga kiwanda chenye teknolojia za kisasa kwa àjili ya  kuchakata mazao ya mifugo, ili  kuimarisha soko la kimataifa la mazao hayo.

Hayo yamesemwa Waziri wa Klimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo wa SMZ , Shamata Shaame Khamis,  wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge inayosimamia Kilimo, Biashara na Utalii kutoka Baraza la Uwakilishi Zanzibar mkoani Tanga.

Alisema kuwa kutokana na kuwa na uhitaji mkubwa wa nyama katika masoko ya kimataifa, hivyo serikali imeona haja ya kujenga kiwanda hicho ambacho kitakuwa na miundombinu ya kisasa Kwa ajili ya kuchakata mazao hayo.

“Ziara yetu mkoani Tanga ni kwa lengo la kujifunza namna bora ya utunzaji wa mifugo pamoja na malisho, ili kupata mazao ambayo yataweza kukidhi vigezo vya masoko ya kimataifa kwa urahisi,”alisema Waziri huyo.

Kamati hiyo ilitembelea pia Kituo cha Utafiti cha Mifugo  (TALIRI), Kanda ya Mashariki kilichopo mkoani hapa kwa ajili ya kujionea teknolojia mbalimbali za malisho bora kwa mifugo.

Kaimu Mkurungenzi wa kituo hicho, Dk Zabron  Nziku alisema kuwa katika kuhakikisha wanamsaidia mfugaji kuweza kupata mazao mengi na yenye tija, wapo katika hatua ya mwisho ya utafiti wa malisho bora kwa àjili ya mifugo iliyoko ukanda wa Pwani.

Habari Zifananazo

Back to top button