Kiwanda cha maziwa chapata tuzo kujali afya za walaji

KIWANDA cha Kuzalisha Maziwa ya Kilimanjaro Fresh kupitia kampuni yake ya Galaxy Food and Beverage ya jijini Arusha kimeibuka mshindi wa kutoa maziwa bora nchini na kutunukiwa tuzo ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika kuhudumia afya za walaji nchini.

Mkurugeni wa Kampuni hiyo, Virjee Saqalain alishukuru ushindi huo na kusema kuwa umempa ari zaidi ya kuimarisha shughuli zake ili kuwafikia wateja wengi zaidi hapa nchini.

Aidha aliwataka wafugaji kutumia fursa ya uwepo wa kiwanda hicho mkoani Arusha kuzalisha maziwa kwa wingi na kuuza kiwandani hapo ili kujiongezea kipato na kunufaika na mifugo yao.

Virjee alisema kuwa kiwanda hicho kimekuwa mkombozi kwa mkulima na wafugaji wa Mkoa wa Arusha na maeneo ya pembezoni kwa kununua bidhaa hiyo na kimeleta tija kwa kupandisha thamani ya maziwa ambapo hapo awali wafugaji walikuwa hawana soko la uhakika.

“Wateja wa bidhaa za maziwa wamechagua kampuni yangu ya Galaxy Food and Beverage kiwanda kinachopendwa zaidi mwaka huu ndio maana tumepata ushindi,Niwaombe wafugaji kuuza maziwa kwetu kupitia vituo vyetu ama kiwanda chetu kilichopo Ungalimited ”

Kampuni hiyo inatengeneza na kusambaza bidhaa mbalimbali za maziwa kwa jina la Kilimanjaro Fresh kwa masoko ya ndani ,katika mikoa ya Arusha Singida,Babati,Manyara ,Shinyanga ,Mwanza na ina bohari Dodoma, Mwanza na Dar es Salaam.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button