TANGA: Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema kuwa kiwango cha upatikanaji wa maji safi na salama nchini ni asilimia 88 kwa mijini huku vijiji ikiwa ni asilimia 77.
Hayo amesema wakati wa uzinduzi wa hatifungani ya kijani ya Mamlaka ya maji Tanga ambapo amesema kuwa mpaka ifikapo Juni 2025 watakuwa wamefikia lengo walilowekewa.
Amesema wakati malengo ya serikali ni kuhakikisha mpaka ifikapo mwaka 2025 kiwango cha maji mijini kiwe asilimia 95 lakini kwa kasi ya utekelezaji wa miradi tutaweza kufikia 100 mijini huku vijijini ikiwa zaidi ya 85
“Fursa hii ya hatifungani inakwenda kuwasuluhisho kwa mamlaka zetu kuweza kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wakati na wananchi kuwasogezea huduma karibu na maeneo yao”amesema Waziri Aweso.
Nae Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji UNCDF Peter Malika amesema kuwa hatifungani ni fursa kwa Tanzania.
“Mpango huu utarahisisha upatikanaji wa fedha za miradi ya maendeleo kwa wakati na zitatikana na wananchi wenye hivyo kusaidia kuimarisha huduma lakini na uchumi wa watu wetu”amesema Malikaa.