Kiwanja cha ndege kujengwa ndani ya hifadhi mikumi

MSIMAMIZI Mkuu wa Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) wa Benki ya Dunia Dk, Enos Esikuri ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kikoboga kinachojengwa ndani ya Hifadhi ya Taifa Mikumi.

Akiwa ameambatana na  wataalam kutoka Benki ya Dunia, pamoja na Watekelezaji wa Mradi  wa REGROW  na  wasimamizi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii Dk ,Esikuri amepongeza hatua nzuri iliyofikiwa ya ujenzi wa uwanja huo wa ndege ambao utakuwa na urefu wa kilomita 2.4

Aidha Dk Esikuri licha ya pongezi alizozitoa amesisitiza wakandarasi kuhakikisha wanamaliza Mradi  kwa wakati uliopangwa na kwa ubora, ili uweze kutumika mapema mwakani na kuwaletea watanzania maendeleo zaidi.

Advertisement

Wakiwa katika Kijiji cha Msolwa Station, Wataalam kutoka Benki ya Dunia wamekutana na Vikundi vya Kijamii (COCOBA) vinavyowezeshwa na Mradi wa REGROW kwa lengo la kupata uwelewa wa pamoja wa maendeleo ya miradi hiyo.

Aidha Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Hemed Mpoto kwa niaba ya wanavijiji wote ameushukuru uongozi huo wa Benki ya Dunia kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea watanzania maendeleo kupitia sekta ya Utalii.

Kijiji cha msolwa station kinajumla ya vikundi 15, vimepatiwa jumla ya fedha mbegu kutoka Mradi wa REGROW kiasi cha sh  milioni 1.3  na  vikundi 15 vimepatiwa fedha za kutekeleza miradi yao kiasi cha Sh milioni 3.5 askari wa wanyamapori wa Vijiji (VGS) 10, na Wanafunzi 94 wamepata ufadhili wa masomo.

 

 

 

 

 

 

 

 

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *