MKAZI wa Tabata Mawenzi, Mohamed Masoli amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akikabiliwa na mashtaka ya usafirishaji wa binadamu kinyume cha sheria.
Mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka hayo mahakamani hapo jana na Wakili wa Serikali, Caroline Matemu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhani Rugemarila.
Matemu alidai Juni 11, 2021 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) alikutwa akimsafirisha Rahma Yusuph kwa kigezo cha kumtafutia kazi nje ya nchi kinyume cha sheria.
Matemu alidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na aliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Novemba 14, mwaka huu na mshitakiwa alipelekwa mahabusu kwa kuwa shtaka linalomkabili halina dhama