Km 497 zimeathiriwa na mvua Dar

DAR ES  SALAAM: MENEJA wa Tarura Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Geofrey Mkinga amesema kilometa 497 mkoani humo zimeathiriwa na mvua zilizoambatana na Elinino zilizoanaza Oktoba 5 ,2023 hadi Mei 2024

Mkinga amesema kutokana na uharibifu huo Tarura Mkoa wa Dar es Salaam imelazimika kukarabati barabara hizo, vivuko na madaraja ili kurudisha mawasiliano ambayo yalikatika kutoka na mvua.

“Kimsingi niseme serikali imejikuta ikiingia katika gharama kubwa za ukarabati wa miundombinu ili kurejesha mawasilino baina ya watu walioathirika na mafuriko ili shughuli za kiuchumi na kijamii ziendelee”amesema Mkinga

Alipotakiwa kuzungumzia kiasi cha fedha kilichotumika katika ukarabati wa miundombinu hiyo amesema kwasasa ni vigumu kueleza takwimu sahihi kwakuwa wahandisi na wakandarasi wapo kazini kwa maana kwamba ukarabati bado unaendelea baada ya mvua kupungua.

SOMA: Sh bilioni 65 zahitajika athari za mvua

Mvua hizo zimesababisha uharibifu ama kusomba madaraja 27, na madaraja 14 yalirejeshwa kwa haraka baada yakutokea kwa mafuriko na mengine yakiendelea kukarabatiwa ambapo matatu bado hayajarejeshwa ambapo bado yanaendelea kukarabatiwa kutokana na kuathiriwa zaidi wakati huohuo 10 yakisubiri mvua zikatike na bila shaka Tarura wameanza kazi hiyo kwakuwa mvua zimekatika kwa kiasi fulani.

Madaraja mengine ambayo hayatumiki na Tarura imefanya mbadala ni pamoja na Daraja la Tasafu wilayani Temeke, Msumi Madale 11 Km kivuko cha watembea kwa miguu mkandarasi yupo kazini.

Hata hivyo Mkinga amewataka wananchi kuwa wavumilivu wakati Tarura wafanyia kazi changamoto za miundombinu ya madaraja kwakuwa Daraja siyo kitu kidogo na cha mzaha bali ni muundombinu muhimu ambao huhitaji umakini wa hali ya juu.

Kwa Daraja la Msumi-Kivule amesema lilikuwa katika hali mbaya zaidi kiasi kwamba lilikuwa linaelea na hivyo kuwekeza nguvu zaidi” Tunakwenda kulifanyia kazi zaidi tunaelewa adha wanayoipata ila watuvumilie halkadharika Pugu Majohe-Mbondole litafanyiwa kazi kwa vipande vipande na kwa upande wa viwege wamejenga madaraja ya muda ya plastiki kwenda kwa mhaya ambapo Sh milioni 350 zimetumika.

“Kwakifupi ndiyo hivyo, serikali imetuagiza tufanye tathimini na mvua bado haitabiriki lakini tunahakikisha mawasiliano yanapatikana na kwakuwa bajeti ya Wizara ya Ujenzi imepita ni Imani yangu mambo yatakuwa murua na barabaraa” amesema Mkinga

Na hivyo ifikapo Julai Mosi wakandarasi wote watakuwa kazini na Barabara ya Kitunda -Kivule itakarabatiwa vizuri pasina shaka.

Baadhi ya wananchi wa maeneo yaliyoathirika wameipongeza serikali nakuishukuru kwa namna ambavyo inashughulikia changamoto za wananchi hususani wakati wa shida na majanga.

 

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button