TIMU ya KMC imejihakikishia kucheza ligi kuu msimu ujao maara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-0 leo hii dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa mtoano mkondo wa pili uliopigwa kwenye dimba la Uhuru Dar es Salaam.
Mabao ya KMC katika mchezo huo yamefungwa na Daruwesh Saliboko dakika ya tatu na Awesu Awesu dakika ya 28 ya mchezo.
Matokeo ya leo yameifanya KMC kuwa na ushindi wa jumla wa mabao 3-2 na kuihakikishia nafasi ya kucheza ligi kuu kwa msimu ujao.
Mbeya City watalazimika kucheza mchezo mwingine dhidi ya Mashujaa ya Kigoma ili kujua hatma yao kwenye ligi kuu kwa msimu ujao.