KMC yaachana na nyota wake tisa

SIKU chache baada ya kumtangaza kocha mpya Abdulhamid Moalin, timu ya KMC imetangaza kuachana na wacheza tisa wa kikosi hicho baada ya kumaliza mikataba yao.

Ofisa habari wa klabu hiyo Christina Mwagala asema tayari wameanza maboresho ya kikosi chao, ili kufanya vizuri msimu ujao kwa kuachana na baadhi ya wachezaji na kusajili wengine.

Kwa mujibu wa Mwagala wachezaji walioachana na timu hiyo baada ya kumaliza mikataba ni mshambuliaji Matheo Antony, makipa Nurdin Balor na, David Kisu, viungo Mohamed Samata, Frank Zakaria ,Issac Kachwele, Kelvin Kijili, Steve Nzigamasabo na Ally Ramadhan.

Amesema tayari timu hiyo imekamilisha usajili wa wachezaji nane ambao ni Wilbol Maseke, Rahimu Shomary, Fredy Tangalo, Vicent Abubakari, Andrew Sinchimba, Juma Shemvuni, Roges Gabriel na Twalib Mohamed.

Kikosi hicho kinatarajia kuingia kambini kesho Julai 15, 2023 kwa maandalizi ya msimu ujao utakaoanza Agost 15, 2023.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button