KMC yamfuta kazi Kocha Mkuu

UONGOZI  wa timu ya KMC FC, umemfuta kazi  Kocha Mkuu wa timu hiyo  Thiery Hitimana pamoja na benchi lote la ufundi kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na HabariLEO, Mwenyekiti wa Bodi ya KMC, Songoro Mnyonge ameeleza kuwa kikosi chao kwa sasa kitakuwa chini ya kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ atakayeiongoza timu hiyo hadi mwisho wa msimu, huku wakimpa nafasi ya kuchagua wasaidizi wake.

“Tumesaliwa na mechi nne kwenye ligi imani yetu ni kwamba Julio atatusaidia kuirudisha timu kwenye nafasi salama,” amesema Mnyonge.

KMC inashika nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 26, ambapo katika michezo 5 ya mwisho ya ligi imeshinda  mmoja pekee, ikifungwa michezo 4.

 

Habari Zifananazo

Back to top button