KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya England, Sven Goran Eriksson ameambiwa na madaktari kuwa amebakisha mwaka mmoja wa kuishi mara baada ya kugundulika kuwa na saratani.
Eriksson, 75, amekiambia kituo kimoja cha redio cha P1 nchini Sweden kuwa: “Kila mtu amebaki anajua nina ugonjwa ambao sio mzuri. Ila natakiwa kupambania afya yangu.”aliaambia P1.
Eriksson alikuwa akikimbia kilomita tano kwa siku kabla ya kwenda hospitalini, alisema kabla ya kuzimia na kuzirai na baadaye ilibainika kuwa alikuwa na saratani.
“Sina maumivu yoyote makubwa. Lakini nimegundulika kuwa na ugonjwa ambao unaweza kupunguza kasi ya kuishi mbaya zaidi huwezi kuufanyia upasuaji.”Aliongeza.
Mwaka 2001 na 2006, Eriksson alifundisha kile kinachoitwa “kizazi cha dhahabu” cha wanasoka katika timu ya Uingereza akiwemo David Beckham, Steven Gerrard, Wayne Rooney na Frank Lampard.