KOCHA wa timu ya taifa ya Gambia, Tom Saintfiet amejiuzulu wadhifa wake baada ya kushindwa kulivusha taifa hilo hatua ya 16 bora ya michuano ya Mataifa ya Afrika.
Hatua hiyo ni baada ya kipigo cha mabao 2-3 dhidi ya Cameroon hatua ya makundi yanayorindima nchini Ivory Coast.
Gambia wameburuza mkia katika Kundi C baada kutovuna alama yoyote katika kundi hilo.
Michezo mitatu mitatu ya kundi hilo yalikuwa katili kwa Gambia, 3-0 vs Senegal, 1-0 vs Guinea na hiko cha leo.
Raia huyu wa Ubelgiji amewahi kuhudumu katika Ligi Kuu Tanzania Bara, msimu wa mwaka 2012-13 akiwa Kocha Mkuu wa Yanga SC.
Ajiunga na Yanga Julai 2012 na akahudumu kwa takribani siku 80 pekee huku akitimuliwa kwa matokeo mabaya, yumkini aliipa taji la michuano ya Kagame.