Kocha Ivory Coast afungashwa virago

TIMU ya taifa ya Ivory Coast imeachana na kocha wake Jean Louis Gasset.

Hatua hiyo ni baada ya timu hiyo kukubali mvua ya mabao 4-0 kutoka kwa Equtorial Guinea katika mchezo wa mwisho wa kundi A uliopigwa Jumatatu Januari 22, 2024.

Kilikuwa ni kipigo kizito zaidi cha nyumbani katika historia ya Ivory Coast na wanakuwa mwenyeji wa kwanza wa Afcon kupoteza michezo miwili ya makundi tangu walipofanya hivyo mwaka 1984.

‘The elephant’ wana matumaini hafifu ya kutinga hatua ya 16 bora kama moja ya timu bora zilizoshika nafasi ya tatu.

Wataongozwa na Emerse Fae, mmoja wa makocha wa Gasset, kwa muda.

Shirikisho la soka nchini humo lilisema “limekatisha kandarasi” ya Gasset mwenye umri wa miaka 70 na msaidizi wake Ghislain Printant “kutokana na matokeo duni”.

 

Habari Zifananazo

Back to top button