Kocha Mamelodi atangaza raha

KOCHA Mkuu wa timu ya  Mamelodi Sundowns, Rulani Mokwena amejinasibu kuishangaza Afrika  leo kwenye mchezo dhidi ya Wydad Athletic Club ya nchini Morroco.

Rulani amesema kama kugekuwa na uwezekano wa kupewa kombe basi timu yake inastahili kwa sababu ana kikosi imara, ambacho kilistahili kufika fainali Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.

“Tulistahili kubeba kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita, kwa sababu nafikiri tulikuwa na kikosi bora sana, lakini huwa inatokea unapata kile unachostahili kwenye maisha na mpira wa miguu umekuwa ukitoa matokeo ya kikatili siku zote na ndivyo maisha yalivyo, ” amesema.

Advertisement

Amesema kuwa hisia walizokuwa nazo baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa zilikuwa sio sawa, kwao kwani walisitahili kufika fainali ya mashindano hayo, hivi sasa wameamua kujitoa na kupambana ili kuchukua kombe African Football League.

“Baada ya kupoteza mchezo wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa hisia zetu hazikuwa sawa, kwani kikosi chetu ni bora na aina ya uchezaji wetu ni mzuri wa kuvutia kuelekea mchezo wetu wa leo naamini tutapata ushindi na kuwa timu ya kwanza Afrika kuchukua kikombe cha AFL,” amesema.

Mamelodi Sundowns inatarajia kuchezafainali ya mkondo wa pili ya AFL dhidi ya Wydad Athletic Club katika dimba la Loftus Versfield, Pretoria Afrika Kusini majira ya saa 10 alasiri.

1 comments

Comments are closed.