TIMU ya soka ya Azam imefikia makubaliano ya kuachana na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Abdihamid Moallin.
“Tumefikia makubaliano ya pande mbili na kocha wetu, Abdihamid Moallin, na msaidizi wake, Omary Nasser, kuachia ngazi kama Kocha Mkuu na Msaidizi mtawalia.
“Hata hivyo, makocha hao wataendelea kubaki kama sehemu ya idara ya ufundi klabuni kwetu katika nafasi nyingine, ambazo tutazitangaza hapo baadaye,” imesema sehemu ya taarifa ya klabu hiyo kwenye ukurasa rasmi wa klabu wa instagram leo Jumatatu Agosti 29, 2022.