Kocha Simba haangalii majina

DAR ES SALAAM: ABDELHAK Benchika, kocha mpya wa Simba hatoangalia ukubwa wa majina ya wachezaji wa timu hiyo, atakayejituma atajihakikishia nafasi.
Benchika aliyewasili jana usiku akitokea Algeria, baada ya kutangazwa kuwa kocha wa timu hiyo siku nne zilizopita amesema kiwango cha mchezaji kitampa nafasi.

Akizungumza na wanahabari leo kocha huyo wa zamani wa USM Alger amesema katika kufanikisha mengi muhimu viongozi, wanachama na mashabiki wafahamu mafanikio yatajengwa na Wanasimba wote.

“Kuna mambo mengi ambayo tayari nayajua na nimekuja na mikakati ambayo tutaifanyia kazi. Kuhusu wachezaji tajua zaidi nikishaanza kazi”
“Kuhusu mashindano ya ndani na kimataifa yote ni muhimu. Mimi ni mpambanaji na nitapambana hadi tutafika”. Benchikha
Advertisement
1 comments

Comments are closed.