Kocha Simba sasa aiota fainali

Kocha Simba sasa aiota fainali

BAADA ya kuiongoza timu ya Simba kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, amesema  ameanza kuvuta harufu ya fainali ya michuano hiyo.

Akizungumza na HabariLEO, kocha huyo ameeleza kuwa  hiyo ni kutokana na kuimarika kwa kikosi chake na mipango mizuri inayofanywa na uongozi wa miamba hiyo ya soka nchini.

“Nilizungumza mwanzoni wakati natua Simba, kila kitu kinawezekana kama kutakuwepo na mipango madhubuti na wachezaji kama watajituma na kuweka malengo mbele, leo hii tupo robo fainali wakati hatukupewa nafasi hiyo baada ya kupoteza mechi mbili za mwanzo,” amesema Robertinho.

Advertisement

Chini ya Mbrazili huyo Simba, imefuzu kwa kishindo hatua ya robo fainali baada ya kuifunga Horoya AC mabao 7-0, huku wakisaliwa na mchezo mmoja mkononi wa kuhitimisha mechi za hatua ya makundi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *