Kocha Simba, wenzake 9 wadakwa na ‘unga’

Kocha wa makipa, Muharami Mohamed

KOCHA wa Makipa wa Klabu ya Simba, Muharami Said Mohamed (40) wa wenzake tisa wamekamatwa na kilo 34.89 za dawa za kulevya aina ya Heroin kwa mujibu wa taarifa ya Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA).

Taarifa iliyotolewa leo Novemba 15, imesema Mohamed, Mkazi wa Kigamboni anashikiliwa na wenzake akiwemo Mmiliki wa Kituo cha Cambiasao Sports Academy, Alhaji Kambi Zubery Seif, Mpwa wake Maulid Mohamed Mzungu ‘Mbonde’ (54) ambaye ni Mkazi wa Kamegele Kisemvule.

Advertisement