Kocha Vipers avunja mkataba, kutua Simba?

WAKATI akihusishwa na kujiunga na timu ya Simba ya Dar es Salaam, Kocha Mkuu wa timu ya Vipers ya nchini Uganda, Robert Oliveira ‘Robertinho’, amevunja mkataba na timu hiyo kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Klabu hiyo imetangaza leo kupitia akaunti rasmi ya klabu hiyo kwamba Oliveira anaondoka kwenye timu hiyo kama Kocha Mkuu na watatangaza mbadala wake.

“Klabu inapenda kumshukuru Robertinho kwa juhudi zake alipokuwa Kocha Mkuu, wakati alipokuwa klabuni na kumtakia mafanikio katika siku zijazo, ” ilieleza taarifa hiyo.

Vipers imeeleza kuwa ndani ya muda mfupi iwezekanavyo itatoka na taarifa kuhusu uongozi wa benchi la ufundi kufuatia kuondoka kwa kocha huyo.

Kuondoka kwa kocha huyo bado kunaleta sintofahamu baada ya taarifa mbalimbali kumhusisha na ujio wa Simba SC ambayo bado haijawa na Kocha Mkuu.

 

Habari Zifananazo

Back to top button