Kodi 20% yashushwa kuvutia uwekezaji

Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi, wananchi Kigamboni

KIGAMBONI, Dar es Salaam: RAIS Samia Suluhu Hassan amesema serikali imepunguza kodi ya makampuni kutoka asilimia 30 hadi 10 kwa kipindi cha miaka mitano ya mwanzo ili kuchochea uwekezaji zaidi kwenye sekta ya viwanda

Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya mojawapo ya Gari lililounganishwa katika Kiwanda cha Kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limitedkilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Mei 09, 2024.

Akihutubia katika uzinduzi wa kiwanda cha kuunganisha malori na matipa cha Saturn Corporation Limited kilichopo Wilaya ya Kigamboni, Mkoa Dar es Salaam leo Mei 9,2024, Rais Samia ameahidi kuwa serikali itaendelea kujenga uchumi wa kisasa, fungamanishi, jumuishi na shindani katika msingi wa viwanda, huduma za kiuchumi na miundombinu wezeshi.

Soma pia: https://www.viwanda.go.tz/news/rais-wa-jamhuri-ya-muungano-wa-tanzania-mhe-samia-suluhu-hassan-amewataka-wawekezaji-katika-viwanda-vya-sukari-nchini-kuchangia-kikamilifu-kufanikisha-malengo-ya-kujitosheleza

Advertisement

Amesema sekta ya viwanda inaongeza uzalishaji na kutoa ajira kwa wananchi,jambo ambalo ni muhimu katika kukuza uchumi jumuishi na kusaidia na kusaidia katika mapambano ya umaskini.

Soma pia: https://habarileo.co.tz/serikali-kufufua-viwanda-vilivyokufa/

Kwa upande mwingine Rais Samia amesema kiwanda hiko kitatoa ajira za moja kwa moja takribani 250 na zisizo za moja kwa moja 1800 kuongeza mzunguko wa fedha,mapato ya serikali na kuhaulisha Teknolojia.