Kolo Toure bossi mpya Wigan

Kolo Toure

BEKI wa zamani wa Arsenal, Kolo Toure ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya Wigan inayoshiriki Ligi ya ‘Championship’ nchini England, akichukuwa nafasi ya Leam Richardson aliyetimuliwa Novemba 10, 2022. Toure amesaini mkataba wa miaka mitatu.

Kolo (41) raia wa Ivory Coast, ambaye amewahi pia kuichezea Man City, alikuwa akifanya kazi kama mkufunzi wa kikosi cha Leicester tangu Februari 2019, alifanya mazungumzo na timu hiyo mapema mwezi huu na sasa amekamilisha uhamisho wake.

Wigan walimtimua kocha huyu baada ya kucheza mechi nane bila ushindi. Baada ya kumchagua Toure kama mrithi wake, afisa mkuu mtendaji wa Wigan Malachy Brannigan alisema: “Tunafuraha kwamba Kolo amekuwa meneja mpya wa Wigan Athletic na bodi inafurahi kwamba yeye ndiye mtu wa kutupeleka mbele.

Advertisement