Kombe la Dunia, Mbashara TBC

ZIKIWA zimebaki siku 30 kwa Kombe la Dunia kuanza kurindimba , Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) litakua mbashara kwa kuonyesha mechi 92 za Kombe hilo nchini Qatar.

Michuano hiyo itaanza rasmi Novemba 20 hadi Desemba 18 ambapo mashabiki wa soka nchini watapata fursa ya kushuhudia mitanange hiyo kupitia TBC One,TBC Radio,TBC Taifa na TBC On line.

Akizungumza leo Oktoba 21,2022, Mkurugenzi wa TBC Ayub Rioba amesema katika michuano hiyo ya Kombe la Dunia jumla ya mechi 28 zitatangazwa kupitia TBC One na TBC online na mechi 64 zitatngazwa kupitia TBC Radio yenye kauli mbiu yake ‘MBUNGI NYUMBANI BUUURE’.

“Hili si jmbo geni kwetu TBC tuna uzoefu mkubwa wa kurusha Kombe la Dunia historia inaonyesha TBC ilishatangaza mashindano haya mwaka 2010, 2014 na fainali za mwaka 2018.” Amesema Rioba

Aidha amesema katika faina za mwaka huu TBC imefanya juhudi kubwa kuhakikisha watanzania wanapata haki ya kuburudika na michuano hiyo mikubwa duniani ambayo ufanyika kila baada ya miaka minne.

Amesema tayari shirika hilo limeanza kurusha vipindi vya matangazo mbalimbali kuhamasisha wasikilizaji na watazamaji wao kuwa tayari kwa michuano hiyo.

“Tuna kipindi cha GOZI QATAR kinachoruka kwenye Televisheni yetu ya TBC One na KIOTA kinachoruka kwenye Radio zetu mbili za TBC Taifa, TBC Fm na TBC Online ambavyo vyote vinazungumzia na kuhamasisha michuano ya Kombe la Dunia,” amesema Rioba.

Pia amesema wanavipengere viwili ambavyo vinaruka kwenye vipindi mbalimbali vya Radio na Televisheni ambavyo vinaitwa Nahodha na Chama langu vinavyozungumzia wachezaji na timu mbalimbali zitakazo shiriki fainali za kombe la hilo la Dunia Qatar 2022.

 

Habari Zifananazo

Back to top button