Kombora lajeruhi wanahabari 11 wa Uturuki

SHAMBULIZI la kombora la Urusi lililolenga hoteli moja katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine wa Kharkiv limejeruhi takriban watu 11, wakiwemo waandishi wa habari wa Uturuki waliokuwa wakiripoti vita hivyo, maafisa wa eneo hilo walisema.

“Tisa kati ya waliojeruhiwa wamepelekwa kwenye vituo vya matibabu,” Gavana wa Mkoa wa Kharkiv, Oleh Synehubov alisema kwenye chaneli yake rasmi ya Telegraph. “Mmoja wao, mwanaume mwenye umri wa miaka 35, yuko katika hali mbaya,” alisema.

Picha na video za shambulio hilo zilionyesha madirisha ya hoteli hiyo yakiwa yamelipuliwa na vipande vya vioo vikiwa vimetapakaa ardhini. Shambulio hilo pia liliharibu balcony, na kufanya kuwa mirundiko mikubwa ya vifusi vya saruji mitaani.

Baadhi ya waandishi wa habari wa Uturuki waliokuwa wakizuru walikuwa miongoni mwa waliojeruhiwa, gavana huyo aliandika.

Habari Zifananazo

Back to top button