MDAHALO wa kumuenzi Mwalimu Julius Nyerere kujadili mfumo wa demokrasia ya vyama vingi unatarajiwa kufanyika kesho jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Taasisi ya The Mwalimu Nyerere, Prof. Francis Matambalya, amesema kuwa mdahalo huo wasiku moja utahusisha wadau mbalimbali na utafanyika New Africa Hotel
“Tutajadili mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, wanaionaje. Wajibu wa viongozi wa vyama vya siasa, nafasi kurasimisha mfumo wa vyama vingi, uhusiano kati ya dola na vyama vya siasa, sera, Katiba, sheria, kanuni na taratibu,” amesema Prof.Matambalya