Kongamano fursa za TEHAMA Tanzania-DRC kuanza Lubumbashi leo

Kongamano la Fursa za Kibiashara na Uwekezaji katika sekta ya TEHAMA linaanza leo, jijini Lubumbashi, DRC.

 

Tukio hilo la siku mbili linaongozwa kaulimbiu: “Kukuza Fursa za Mashirikiano, Biashara na Uwekezaji katika sekta ya TEHAMA”

Advertisement

Wageni Rasmi katika Kongamano hilo ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kutoka Tanzania, Nape Nnauye na Waziri wa Posta, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Augustin Kibassa Maliba.

Washiriki zaidi ya 300 wanatarajiwa kushiriki Kongamano hilo la siku mbili.

 

Augustin Maliba, Waziri wa Posta, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Taasisi za Tanzania zinazoshiriki ni pamoja na TAnTRADE, TTCL, Shirika la Posta, Mamlaka ya Serikali MtandaoTanzania, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki na TPSF.