Kongamano kujadili teknolojia ya akili bandia laja

DSM; TUME ya Tehama (ICTC), imesema teknolojia ibukizi ya akili bandia imekuwa na changamoto kubwa duniani, jambo linalohitaji mjadala wa kina nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa ICTC, Dk Nkundwe Mwasaga amesema hayo leo Dar es Salaam wakati akisaini hati ya makubaliano ya kukuza ubunifu wa Tehama kwa wanawake nchini pamoja na kuanzisha kampuni za kufanya kazi mitandaoni.

Makubaliano hayo amesaini na taasisi ya HiPiPo ya nchini Uganda chini ya Ofisa Mtendaji Mkuu,Innocent Kawooya.

Kuhusu akili bandia amesema ni moja ya mada itakayojadiliwa katika kongamano la saba la Tehama linalitarajiwa kufanyika nchini kuanzia Oktoba 16-20, mwaka huu.

Amesema washiriki watajadili mafanikio na changamoto za Tehama kwa wanawake na vijana na kuzipatia suluhu, lakini pia kuona namna wanavyoweza kushirikiana na kanda mbalimbali katika kuleta maendeleo.

Amesema suala la teknolojia ya ibukizi ya akili bandia inahitaji kuwa na ujuzi wa kidijitali wa kutosha, kuwepo kwa watalam ambao watakuwa wamepewa mafunzo lakini pia kuangalia suala zima la usalama wa miundombinu ya Tehama na uchumi wa kidijitali.

Amesema kongamano hilo litajadili na kuona ni kwa namna gani mapinduzi ya teknolojia yanavyoweza kuongeza pato la Taifa.

Kuhusu kwa nini wanawake ndio walengwa wakuu, amesema hatua hiyo ni katika kuwa na uchumi jumuishi kwamba kundi hilo liweze kunufaika na mabadiliko ya teknolojia.

“Siku za mwanzoni wanaume walifanikiwa zaidi katika nyanja ya teknolojia, lakini mafanikio ya sasa yanatakiwa kuwa na ujumuishi,” amesema nakuongeza kuwa kongamano linatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 300.

Kahusu makubaliano ameseman alenga kuwezesha Tehama iwatengeneze wanawake kuwa na nafasi kubwa ya kufanya kazi na kuchangia katika pato la Taifa.

Habari Zifananazo

Back to top button