Kongamano la biashara China, Tanzania laiva

ZAIDI ya Taasisi 50 zinatarajiwa kushiriki Kongamano la Biashara la Kimataifa  lililoandaliwa na Jukwaa lijulikanalo kama ‘China Trade Week’ (CTW) na kuwahusisha wafanyabiashara mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

Kongamano hilo litakalohusisha maonesho zaidi ya bidhaa 200, zikiwemo za kielektroniki, viwanda, afya, nguo, mavazi, urembo na ujenzi litafanyika  Septemba 26 hadi 28 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa waandaaji wa kongamano hilo, Zahor Ahmed, tukio Hilo linalofanyika kwa mara ya kwanza nchini pamoja na mambo mengine limelenga kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na China.

” Pamoja na sababu zingine kongamano hilo limelenga kufungua  uchumi wa kimataifa kwa mataifa haya mawili na dunia nzima, biashara itakuwa mstari wa mbele kuleta maendeleo ya kitaifa,” amesema Ahmed.

Amesema kongamano  hilo ambalo Tanzania itakuwa taifa la sita kuwa mwenyeji limeshafanyika katika nchi za Kenya, Ethiopia, Ghana, Morocco na Afrika Kusini yakijumuisha maonesho ya bidhaa mbalimbali.

Mbali na faida  za  kiuchumi, kongamano hilo pia litasaidia uwekezaji na kubadilishana tamaduni zilizohusu sekta za ujenzi wa miundombinu, nishati, kilimo, chakula, sayansi na teknolojia.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button