Kongamano la C2C lafanyika Dar

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Jim Yonazi akishiriki kongamano la kuunganisha wadau wa TEHAMA wakiwemo wa Miundombinu wa Ndani na Nje ya Nchi ‘Connect 2 Connect - C2C’ linaloendelea leo Septemba 8, 2022 katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo lilifunguliwa jana na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (Mb) na linatarajiwa kufungwa leo na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Khalid Suleiman Mohamed.