Kongani kukuza ujuzi kwa vijana

KAGERA: KUANZISHWA kwa kongani ya vijana katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kimekuwa kichocheo cha ukuaji wa shughuli za kiuchumi kwa vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za ufundi ambazo zinawaingizia kipato.

Utekelezaji wa Sera ya Vijana ya Mwaka 2017 hadi 2034 imeisukuma Manispaa ya Bukoba kutenga zaidi ya Sh milioni 374 kujenga kongani kubwa ambayo sasa imeukusanya vikundi vinane vya vijana 78 wanaojishughulisha na maswala ya ufundi kwa kutumia kongani hiyo kama sehemu kubwa ya kujiingizia kipato na kubadilishana uzoefu.

Ofisa vijana wa Manispaa ya Bukoba Suzana Majule ametoa taarifa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ismail Ussi na kudai kuwa lengo la Manispaa ya Bukoba ni kuhakikisha vijana wanajipatia ajira lakini kongani hiyo inatumika kama chuo cha maarifa ya kutoa ujuzi kwa vijana walioko mitaani.

Amesema nje ya vijana 78 waliopo hapo tayari wamepokea wanafunzi walikotoka Mtaani na vikundi vinne vimepata Mkopo wa asilimia 10 kutoka Manispaa ya Bukoba Kwa ajili ya kuendesha shughuli zao.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa amepata fursa ya kukimbiza Mwenge wa Uhuru katika Manispaa ya Bukoba na kumweleza Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru kuwa kongani za vijana sasa katika mkoa wa Kagera zimefikia tano kwenye hallmashauri mbalimbali Kagera.

Amesema matamanio yake ni kuona kila anapata fursa ya kujiajili na kupata ujuzi wa kumwinua mwingine kupitia Kongani hizo na kuhaidi kuwa mkoa utasimamia swala hilo kwa nguvu zote na kila Halmashauri ya Kagera itapata kongani ya kuongeza ujuzi kwa vijana.

“Kama mkuu wa mkoa nimejigawa kuhakisha Kila sekta inayogusa vijana inatumika vyema nataka katika kilimo vijana wawemo,ufugaji wawemo ,ufundi wawemo ujuzi wawemo ili swala la mtu kuomba elfu 30 nalichukia sana ,natamani vijana wajiajiri kupitia udhubutu na utaalamu wao ambao utawafikisha mbali,” amesema Mwassa.

Ismail Ussi amepongeza ubunifu wa viongozi wa Manispaa ya Bukoba Kwa kutekeleza sera za vijana na kudai kuwa vijana wengi wanayo maono ya kufanya mambo makubwa changamoto kubwa ni mitaji na maeneo ya kufanyia kazi zao na kuonyesha vipaji vyao.

Amesema kongani ambayo imewekewa Jiwe la Msingi baada ya kukamilika kwake itaongeza mshikamano kwa vijana na baada ya miaka mitano kongani hiyo itakuwa moja ya vyuo vinavyohitimisha vijana wenye uwezo mkubwa katika maswala ya ufundi na maswala ya tekinolojia

Ametoa wito kwa vijana kuwa wanyekevu na kujifunza kwa uaminifu na ubunifu ili waweze kutumikia vipaji vyao na kuvionyesha adharani na jamii iweze kuwaamini na njia hiyo itawafanya kuwa taa na kutimiza malengo na sera ya serikali.

Mwenge wa Uhuru umezindua katika Manispaa ya Bukoba imetenbelea kuzindua kukagua na kuweka mawe ya Msingi katika miradi Saba yenye thamani ya Sh bilioni 5.7.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button