TAASISI ya Wakorea inayoitwa Kofih Tanzania imeingia mkataba wa ushirikiano kwa miaka mitano na hospitali ya wilaya ya Chalinze.
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete amesema kuwa makubaliano hayo yatawezesha kuimarishwa kwa miundombinu ya Afya hasa Hospitali ya Wilaya, vituo Vya Afya na kuwezesha vifaa tiba katika eneo la wakina mama na Watoto.
Amesema, pia mahitaji ya vifaa vya huduma za dharura na kuwezesha watendaji wa sekta mafunzo ya ujuzi wa juu katika Halmashauri hiyo.
Comments are closed.