Korea Kusini yapiga marufuku ulaji nyama ya mbwa

BUNGE nchini Korea Kusini limepitisha sheria mpya inayolenga kukomesha uchinjaji na uuzaji wa nyama ya mbwa ifikapo 2027.

Sheria hiyo inalenga kukomesha utamaduni ambao baadhi ya wanaharakati wa taifa hilo wameiita ni aibu kwa nchi hiyo.

Chini ya sheria hiyo, kufuga au kuchinja mbwa kwa ajili ya kuliwa kutapigwa marufuku, vile vile kusambaza au kuuza nyama ya mbwa hata hivyo watakaopatikana na hatia ya kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria.

jela.

Sheria hiyo inasema ufugaji, muuzaji na mchinjaji wa mbwa kwa ajili ya nyama ataadhibiwa hadi miaka mitatu jela au faini ya Won milioni 30 ($23,000).

Nyama ya mbwa kwa muda mrefu imekuwa sehemu ya vyakula vya Korea Kusini, na kwa wakati mmoja mbwa milioni moja wanaaminika kuuawa kwa biashara hiyo kila mwaka.

Lakini ulaji umepungua kwa miezi ya hivi karibuni.

Kulingana na takwimu za serikali, Korea Kusini ilikuwa na karibu vibanda 1,600 vya nyama ya mbwa na mashamba 1,150 ya mbwa kufikia 2023.

Habari Zifananazo

Back to top button