Korokoroni kwa kumuua mdogo wake

JESHI la Polisi Mkoani Mwanza linamshikilia Asteria Renatus (34) mkulima na mkazi wa Kitongoji cha Mwajuli Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza kwa tuhuma za kumuua mdogo wake kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali (Sululu) .

Akizungumza na Waandishi wa habari Januari 22,2024 Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza Wilbrod Mutafungwa amesema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 21, 2024 majira ya saa sita kamili mchana katika hospitali ya Sumve  iliyopo wilayani  Kwimba  ambapo Mlingwa Renatus (15) mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Mwampulu alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.

Mwanafunzi huyo alishambuliwa na  Asteria Renatus ambaye ni dada yake.

“Inadaiwa wazazi ambao ni Renatus Nicholas (64) na mkewe Julitha Ngwanchele (49) pamoja na watoto wengine walikua wameenda shambani kwaajili ya kilimo na kumuacha Asteria akiwa na mdogo wake ndipo alipotenda ukatili huo.

Mtuhumiwa  anaendelea kuhojiwa ikiwa ni pamoja na kujua utimamu wake wa akili na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Habari Zifananazo

Back to top button