Makapi ya korosho dili ya kuzalisha mafuta, umeme

Korosho zote kubanguliwa nchini

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde amesema mkakati wa serikali ni kuhakikisha korosho zote zinabanguliwa nchini ifikapo 2026 ili kukuza sekta ya zao hilo.

Aidha, Mavunde amewataka  wakulima wa korosho kutotupa makapi ya korosho mara baada ya kubanguliwa kwa kuwa makapi hayo ni dili ya kutengeneza mafuta ya meli na kuzalisha umeme.

Mavunde ameyasema hayo alipotembelea viwanda viwili vya Tan- Ko Mirae Green Co. Ltd na Sabayi Investiment vya kubangua korosho na kukamua makapi ya korosho vilivyopo Mkuranga mkoani Pwani.

“Ni maelekezo na dhamira njema na maono ya Mh Rais ya kukuza sekta ya kilimo ifikapo 2030 tayari serikali imetenga bajeti ya sh bilioni 50 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajili ya kuboresha kilimo cha zao la korosho nchini.”Amesema Mavunde

Amesema, tayari serikali imetenga eneo la kutosha kwa ajili hiyo katika kijiji cha Maranje Kata ya Mtiniko Halmashauri ya Mji wa Nanyamba Mkoani Mtwara lenye ukubwa wa Ekari 1375 zimetengwa na zitatumika kujenga kongani ya viwanda

Kwa upande wa Meneja Uendeshaji  wa Kiwanda cha Tan – Ko Green Mirae, Erick Nkanda  amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuchakata tani 8000 za maganda ya korosho ambayo uzalisha mafuta mazito yanayosafirishwa nje ya nchi hususani Korea kwa ajili ya matumizi ya kuzalisha umeme megawati 500 na kusukuma mitambo ya kwenye meli.

Pia,  ujenzi wa kiwanda kingine cha kubangua korosho tani 6000 kwa mwaka unaendelea.

Nae, Mkurugenzi wa Sabayi Investiment, Daniel Marwa amesema kiwanda hicho kimeajiri takribani wanachi 300 ambapo asilimia 80 ni wanawake, huku zaidi ya  wakulima 2000 ndani ya Mkuranga na nje wananufaika na uwepo wa kiwanda hicho.

Amesema, mwaka huu wamebangua   tani 1,000 za korosho kwa  mwaka huu, msimu ujao wanatarajia kubangua tani 10,000 kwa mwaka.

“Sapoti tunayopewa na serikali kupitia Wizara ya Kilimo tunampango wa kufikia tani 40,000 ndani ya miaka mitatu ijayo, bado tunaendelea na uwekezaji, lengo ni kushirikiana na serikali kuhakikisha mwaka 2026 walahu tuwe na uwezo wa kubangua korosho zote hapa hapa nchini,”amesema na kuongeza

“Sisi kama Sabayi tutafanya kwa upande wetu, naamini na wabanguaji wengine nao watafanya kwa nafasi yao, tuna fursa nyingi tunazikosa kwa kushindwa kubangua korosho zetu sisi wenyewe.”Amesema

Nae Meneja wa tawi la Bodi ya Korosho Mkoa wa Dar es Salaam anayesimamia pia Mkoa wa Pwani, Dorina Mkangala amesema bodi ya Korosho inahamasisha ubanguaji wa ndani nchini ili kuhakikisha wanapunguza kiasi cha korosho ghafi kubanguliwa nje, kama mlivyosikia asilimia 90 zinabanguliwa nje ya nchi lengo letu ni kuhakikisha 2026 tunamaliza tatizo hilo.

Amesema kwa sasa kuna viwanda 30 nchini ambavyo vinajihusisha na ubanguaji wa Korosho ambavyo vinauwezo wa kubangua tani 60,000 kila mwaka.

“Huko nyuma wabanguaji walikuwa wanashindana na wanunuzi wa korosho ghafi huko nje ya nchi, lakini tangu mwaka 2021 tuliamua kuwapa soko ‘special’(maalum) wabanguaji wa ndani ambao wanauwezo wa kununua  moja kwa moja kwa mkulima.”Amesema

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Hadija Nasri amewataka wakulima wa zao hilo kuchangamkia fursa zilizopo wilayani hapo.

Habari Zifananazo

Back to top button