Kortini wakidaiwa kuiba mashuka, taulo

WAKAZI wa Dar es Salaam, Johnson Fanuel (42) na Ally Kindimba (52), wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo wakikabiliwa na mashtaka ya wizi wa mashuka, taulo na baiskeli vyenye thamani ya Sh 2,145,000 mali ya mlalamikaji, Neema Samweli.

Washtakiwa hao walisomewa mashitaka yao jana na karani wa mahakama hiyo, Emmy Mwansasu mbele ya Hakimu Gladness Njau.

Mwansasu alidai kuwa watuhumiwa hao katika tarehe isiyofahamika kati ya mwaka 2021 na 2023 wakiwa Mkoa wa Dar es Salaam waliiba vitu hivyo kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Advertisement

Washitakiwa walikana mashitaka yao na kuwekwa mahabusu hadi Julai 20, mwaka huu.

/* */