MUDA wowote kuanzia sasa beki wa Chelsea, Kalidou Koulibaly atajiunga na Al Hilal ya Saudia Arabia.
Taarifa iliyochapishwa muda huu na Fabrizio Romano imeeleza makubaliano ya pande zote tatu, Chelsea, Koulibaly na Al Hilal yamekaa vizuri.
Makubaliano ya mchezaji na Al Hilal yameafikiwa juu ya mkataba wa miaka mitatu.
Amesema mikataba inaendelea kuangalia na baadaye kusainiwa. Beki huyo wa Senegal atakutana na Ruben Neves aliyejiunga kutokea Wolves.
Comments are closed.