KQ yaahirisha makumi ya safari kufuatia mgomo wa marubani
MAKUMI ya safari za ndege za Shirika la ndege la Kenya Airways (KQ) zilizokuwa zimepangwa Jumamosi zimeahirishwa baada ya marubani kuanza mgomo wakishinikiza kurejeshewe pensheni zao ziliizoondolewa na KQ.
Chama cha Marubani Kenya (KALPA) kimesema marubani hawata rejea kazini ikiwa viongozi wa KQ hawatatii takwa hilo. Waziri wa Uchukuzi nchini Kenya, Kipchumba Murkomen na Menejimenti ya Shirika hilo la ndege wamesema mgomo huo ni batiri na “uhujumu uchumi” kwa taifa la Kenya.
Siku ya Ijumaa, shirika hilo la ndege lilionyesha kwamba hatua za kiviwanda za marubani zinaweza kupoteza angalau Sh bilioni 575.8 karibu (Sh300 milioni) kila siku.
Shirika la ndege la Kenya Airways awali lilikuwa limesema kuwa wako tayari kushirikiana na Chama cha Marubani wa Mashirika ya Ndege ya Kenya (KALPA) kufuatia notisi ya mgomo huo.
Kulingana na meneja mkuu wa KQ Allan Kilavuka, mgomo huo usio halali utasababisha hasara kubwa katika hali ya kifedha ya kampuni hiyo.
“Kwa uchache, hatua isiyo halali ya kiviwanda itagharimu KQ takriban Sh300 milioni (za Kenya) kwa siku, na hivyo kutafsiri Sh2.1 bilioni katika wiki moja,” alisema.
Kilavuka aliongeza kuwa kampuni imepiga hatua katika kuboresha hali yake ya kifedha kufuatia janga la UVIKO-19, na hatua ya KALPA itapuuza juhudi hizo.
Alisisitiza kuwa mgomo huo ni kinyume cha sheria, unakuja wakati mbaya na hauhitajiki.
“Kitendo hiki cha kusikitisha kinaweza kuathiri abiria wetu ambao hawawezi kusafiri, na wateja wetu wa mizigo, ambao mauzo yao ya nje yataathiriwa. Itawasumbua sana wasafiri kwa biashara, matibabu, burudani, na wale wanaoungana na wapendwa wao. Hii inaweza pia kusababisha hasara kubwa kwa wakulima ambao bidhaa zao zinaharibika kwa kucheleweshwa katika soko la nje ya nchi.