Kramo ataja kilichomleta Simba

KIUNGO mshambuliaji wa Simba SC, Aubin Kramo amesema kilichomshawishi kujiunga na timu hiyo ni ubora na dhamira katika kupambana kuwa shindani Afrika. Kauli hiyo ameitoa leo alipokuwa kwenye mahojiano na Simba TV

“Meneja wangu alinipigia simu na kuniambia kuna ofa ya Simba, nilifikiria kwanza kwakuwa mezani tayari kulikuwa na ofa ya Raja CA (Morocco) na Esperance (Tunisia) lakini ‘vision’ na dhamira ya klabu hiyo katika kutwaa makombe ilinivutia zaidi.” amesema Kramo.

Alipoulizwa kuhusu namna alivyojiandaa na ushindani wa namba, Kramo amesema ni kawaida kwa klabu kubwa kuwa na wachezaji wazuri na ndio maana Simba ilifika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na yeye amejiandaa kutoa alichonacho kwaajili ya kuisaidia klabu hiyo.

Aidha, Kramo amesema licha ya yeye kuwa mchezaji mzuri lakini siku zote akiwa klabuni dhamira yake ya kwanza ni klabu kufanikiwa zaidi kuliko mafanikio binafsi.

Kramo ni winga wa kushoto wa timu ya taifa ya Cote d’Ivoire na amejiunga na Simba katika dirisha kubwa la mwaka huu akitokea Asec Mimosas.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button