Kroos aongeza mwaka mmoja Real Madrid

HISPANIA, Madrid: KIUNGO wa Real Madrid, Toni Kroos, ameamua kusalia katika klabu hiyo kwa msimu mmoja zaidi.

Mtaalamu wa masuala ya uhamisho wa wanamichezo, Fabrizio Romano, aliandika katika ukurasa wake wa X Jumatano kwamba: “Toni Kroos atasalia na kuendelea kucheza Real Madrid kama mkataba mpya wa mwaka mmoja hadi 2025 .

“Mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Kroos na Real Madrid umebaki utaratibu tu wa kusaini. “Msimu huu ni bora sana kwa Kroos hata alipokuwa timu ya taifa ya Ujerumani ameonyesha uwezo mkubwa sana.” ameeleza Fabrizio.

Kroos alijiunga na wababe hao wa La Liga akitokea kwa miamba ya Ujerumani Bayern Munich mwaka 2014.

Tangu wakati huo, Mjerumani huyo ameshinda mataji 20, yakiwemo mataji matatu ya La Liga na manne ya UEFA.

Habari Zifananazo

Back to top button