Kroos kuondoka, kubaki yeye tu
SUALA la kiungo Toni Kroos kuongeza mkataba au kuondoka Real Madrid linabaki upande wake, kwa mujibu wa kocha wa timu hiyo Carlo Anceloti.
Kroos alijiunga na ‘Los Blancos’ 2014 akitokea Bayern Munchen na kusaini mkataba wa miaka sita mwaka jana aliongeza msimu mmoja.
“Ni yeye tu anayeamua. Ni juu ya Toni. Ataamua kwa wakati unaofaa na kwa njia bora, nina uhakika”. Amesema Anceloti.
Mkataba wa sasa wa Toni unamalizika mwezi Juni mwaka huu.