MTWARA: SERIKALI imesema korosho zote zinazozalishwa katika mikoa mbalimbali inayolima zao hilo zitabanguliwa hapa nchini ifikapo mwaka 2030.
Akizungumza mkoani mtwara, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Francis Alfred amesema kila mwaka wamekuwa wakifanya tathimini ya jinsi hali inavyokwenda katika suala la ubanguaji.
‘’Lengo la serikali ni kwamba hadi ifikapo mwaka 2023, lengo letu ni kwamba tuwe tunabangua korosho zote zinazozalishwa hapa nchini”
“Kwahiyo kila mwaka tumekuwa tukifanya tathimini ya jinsi hali inavyokwenda katika ubanguaji, je ikoje’’amesema Alfred
Amesema mwaka 2021 kabla ya kuanza kwa soko la awali walikuwa wakibangua tani elfu 2,000 kwa mwaka.
Kuanzia mwaka 2021/22 walipoanza soko hilo la awali ambapo ubanguaji umeongezeka kutoka tani elfu 4,400 mpaka kufikia tani elfu 26,600 mwaka 2023/24 ingawa bado haujaisha lakini wameanza kupiga hatua kwenda kwenye ubanguaji.
Mfumo huo wa soko la awali ulianzishwa msimu wa mwaka 2021/22 ikiwa moja ya mikakati ya serikali katika kuhamasisha ubanguaji wa korosho nchini na kuwawezesha wabanguaji wa ndani kununua korosho ghafi.