7 wasimamishwa kukatika umeme Uwanja Mkapa

WAFANYAKAZI saba wa Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam wamesimamishwa kazi kutokana na kukatika kwa umeme kwenye uwanja huo wakati wa mchezo wa Yanga na River United ya Nigeria.

Katika mchezo huo uliochezwa jana usiku, Majenereta ya Uwanja wa Mkapa yalileta itilafu na kushindwa kufanya kazi katikati ya mechi ya Yanga na Rivers United ya Nigeria na taa kuzimika kitendo ambacho kilipelekea mchezo usimame kwa zaidi ya dakika 15.

Taarifa ya Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni, Pindi Chana iliyotolewa leo Mei Mosi, 2023 inasema kuwa waliosimamishwa kazi ni Salum Mtumbuka ambaye ni Kaimu Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Manyori Juma Kapesa ambaye ni Mhandisi wa Umeme wa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Tuswege Nikupala ambaye ni Ofisa Tawala Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Said Yakubu akitekeleza agizo la Dk Pindi, pia amewasimamisha kazi kupisha uchunguzi watumishi wengine wanne ambao pia wana majukumu ya uendeshaji wa uwanja hapo.

Watumishi hao ni Gordon Nsajigwa Mwangamilo, Gabriel Mwasele, Yanuaria Imboru na Dkt. Christina Luambano.

Aidha, Wizara imemteua Milinde Mahona kuwa Kaimu Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa na uteuzi huo unaanza mara moja kuanzia leo Mei Mosi,2023.

Taarifa hiyo inasema serikali inawasiliana na wadau wote husika ili mechi zitakazochezwa katika uwanja huo zichezwe wakati wa alasiri badala ya usiku katika kipindi ambacho Wizara inakamilisha taratibu za kupata Mzabuni atakayefanya ukarabati mkubwa katika uwanja huo kabla ya kuanza kwa msimu ujao wa ligi na michuano ya  kimataifa.

 

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
trackback
4 months ago

[…] post Kukati umeme uwanja wa Taifa, 7 wasimamishwa first appeared on […]

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x