‘Kukosekana takwimu sahihi kunaathiri wenye ulemavu’

Viongozi wa Chama cha Watu wenye Ulemavu Shinyanga

MWENYEKITI wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu  mkoani Shinyanga (Shivyawata),  Richard Mpongo, amesema wamekuwa wakishindwa kusaidiwa kikamilifu kwa sababu ya kukosekana takwimu sahihi.

Mpongo amesema hayo leo mbele ya waandishi wa habari na kueleza kuwa awali takwimu walikuwa wakizibuni na kusikitishwa na kitendo cha baadhi ya walemavu kukataa kuhesabiwa.

“Walemavu hawa hawaishi kisiwani, bali kuna watu waliowazunguka, wawape elimu kuhusu masuala ya sense, pale inapoonekana wanagoma kuhesabiwa,” amesema Mpongo.

Advertisement

/* */