Kuku waadimika msimu wa sikukuu

UPATIKANAJI wa kuku katika Soko la Kisutu mkoani Dar es Salaam, umekuwa adimu katika kipindi hiki cha sikukuu kutokana na wafugaji wengi kwenda likizo.

Mwenyekiti wa Wachinjaji Kuku katika soko hilo, Zuberi Mtima amesema hayo alipozungumza na HabariLeo.

Mtima amesema,”Katika msimu huu wa sikukuu kuku walihitajika sana isipokuwa wamekuwa wachache na wadogo wadogo mno.

Advertisement

” Na ule udogo bado unaendelea sio katika ile hali ya uhalisia. Kuku wameadimika na walioko hawakidhi kwa kuwa ni wadogo,”.

Amesema mbali na wafugaji kusafiri msimu huu wa sikukuu, pia hakuna kampuni kubwa za ufugaji za kukidhi mahitaji ya soko hilo kila siku.

Naye Makamu Mwenyekiti katika soko hilo, Shaban Mgweno amesema ni ukweli kuwa msimu wa sikukuu kila mwaka mahitaji ya kuku yamekuwa ni makubwa kuliko uzalishaji.

Amesema pia vifaranga vipo lakini bei za vyakula ziko juu hivyo wafugaji kuamua kufuga kuku wachache.