PAKISTAN: SIKU kama ya leo tunarudi nyuma miaka 35, hadi Novemba 16, 1988 nchini Pakistan ambapo Benazir Bhutto, akachaguliwa kuwa Waziri Mkuu wakwanza mwanamke wa Pakistan. Akihudumu kama Waziri Mkuu kuanzia 1988 hadi 1990 na tena kuanzia 1993 hadi 1996 kupitia Chama cha ‘Pakistan People’s Party (PPP)’.
Alizaliwa Juni 21, 1953 nchini Pakistan na kuuawa katika shambulizi la Desemba 27, 2007 akiwa katika kampeni za nchini mwake.
Benazir ni mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Zulfikar Ali Bhutto anakumbukwa kuwa muwanzilishi wa chama cha PPP, kilichomuweka binti yake madarakani.
Comments are closed.