Kumenoga Hifadhi ya Taifa ya Nyerere

HIFADHI ya Taifa Nyerere (zamani Selous), imekuwa kivutio cha wa watalii wengi kutoka ndani na nje ya nchi, kwa utalii wa boti na upigaji picha wa vivutio mbalimbali vilivyopo majini na pembezoni mwa mto Tufiji.

Akizungumzia sababu ya wengi kuvutiwa na utalii, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Mkuu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Nyerere, Ephrahim Mwangomo amesema viivutio vingi vilivyopo, miundombinu rafiki na ukubwa wa hifadhi unatoa fursa kwa watalii ya kutokusanyika eneo moja kuona vivutio.

Kamisheni Msaidizi Mwangoma ameongeza kuwa, kupitia Mradi wa Kukuza na Kuendeleza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW), hifadhi imepata magari, vifaa mbalimbali kwa ajili ya uhifadhi, mitambo ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu, ili kuimarisha mvuto wa hifadhi kwa wageni wanapotembelea.

Advertisement

Akizungumzia uzoefu alioupata katika hifadhi hiyo, mtalii Wendy kutoka Marekani, amesema ni zaidi ya matarajio yake na watoto wake kuona vivutio vingi ndani ya mazingira yanayovutia sana na kuwa Balozi mzuri wa kuwashawishi ndugu na marafiki zake kutembelea Hifadhi ya Taifa Nyerere.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *