Kumsemea Samia isiwe kichaka cha uhalifu-Mramba

KIBAHA, Pwani: KATIBU wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani, David Mramba, amesema taasisi na mashirika yanayoanzishwa kuisemea serikali na Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Samia Hassan Suluhu yanatakiwa kuhakikisha hayatumiki kama kichaka cha uhalifu.

Mramba ametoa rai hiyo mwishoni mwa juma alipokutanisha mashirika yasio ya kiserikali zenyemrengo mmoja wa kuisemea serikali  na chama na kusisitiza uzalendo kwa wananchi zinazofanya kazi zake katika Mkoa wa Pwani.

SOMA: Kinana aonya wanaomtusi Rais Samia

Katibu huyo amesema yapo baadhi ya mashirika yamegeuka kichaka cha kuhifadhi maovu, kwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na malengo ya uanzishwaji na kuchafua Serikali na chama twala jambo ambalo sio halipendezi kwa jamii.

Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani, David Mramba

Mramba ameagiza Mashirika hayo kufanya kazi kwa manufaa ya taifa na si kujinufaisha yenyewe huku akionya kujiingiza kwenye migogoro ya wagombea nafasi mbalimbali za uongozi katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2025.

“Fanyeni kazi za Taasisi zenu kwa bidii na ubadhilifu mkizingatia lengo la kuanzishwa kwake, msiingie kwenye Taasisi kufuata uteuzi,” amesema Mramba.

Mramba aliyakumbusha mashirika hayo kuhakikisha yanajisajili hadi ifikapo Juni mwaka huu Ili yatambulike kile wanachokifanya.

Kadhalika alisema katika Mkoa huo ipo miradi mingi imetekelezwa na kutokana na hali hiyo katika uchaguzi

Mkuu fomu ya Rais kutoka chama hicho itakuwa kwa ajili ya Dk Samia Suluhu Hassan Ili aendeleze alipoishia kwenye miradi ya maendeleo.

Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Morogoro, Zagina Shanang amewakumbusha wanachama wa chama hicho kuelekea chaguzi zijazo kuhakikisha wanachagua viongozi ambao wanashughuli za kuwaingizia kipato.

Shanang pia ameonya mashirika hayo kuepuka ubaguzi na kutengeneza makundi ya wagombea huku akisisitiza Wanawake kupewa nafasi zaidi za uongozi.

Mmoja wa washiriki wa mkutano huo ulioambatana na mafunzo, Mohamed Mzimba alimpongeza Katibu huyo wa Siasa Uenezi na Mafunzo kwa kuyakutanisha mashirika hayo na kujadili kwa pamoja mambo ya kukijenga chama na Taifa kwa ujumla.

Habari Zifananazo

Back to top button