‘Kuna maeneo 24 ya SEZ’

NAIBU Waziri Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema kwa sasa Programu ya Maeneo Maalum ya Kiuchumi (SEZ), Maeneo Maalum ya Uzalishaji wa Mauzo ya Nje (EPZ) ina jumla ya maeneo 24 ambayo yametangazwa kuwa Maeneo Maalum ya Uwekezaji (SEZ).

Kigahe ameyasema hayo leo jijini hapa wakati wa kujibu swali la msingi la Mbunge wa Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika (CCM), aliyetaka kujua ni lini Serikali itaanzisha  SEZ, ili kuchochea viwanda vya uchakataji Njombe Mjini.

Akijibu swali hilo, Kigahe amesema kuwa kwa sasa Programu ya SEZ/ EPZ ina jumla ya maeneo 24 ambayo yametangazwa kuwa maeneo ya SEZ.

Amesema kuwa Serikali imeendelea na jitihada za kuanzisha Kanda Maalum za Kiuchumi katika maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa uchumi.

“Katika kufanikisha azma hii, Mamlaka ya EPZ imekuwa ikizihamasisha Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kutenga na kuwezesha uendelezaji wa maeneo ya SEZ.”

Kigahe ameongeza kuwa: “Mamlaka ya EPZ iko tayari kushirikiana na Mheshimiwa Mbunge wa Njombe na Uongozi wa Mkoa wa Njombe kufanikisha uanzishaji wa Kanda Maalum ya Kiuchumi katika Mkoa huo.”

Habari Zifananazo

Back to top button