Kuna unyonyaji vyama vya ushirika

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeagiza vyama vya ushirika vitizamwe kwa jicho la pili kwa kile kilichoelezwa kuwa ni vya kinyonyaji.

pharmacy

Maagizo hayo yalitolewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulraman Kinana alipowasili wilayani Muleba mkoani Kagera Ijumaa Septemba 2,2022 kwa ziara ya siku mbili ya kukagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na serikali ikiwa ni pamoja na kukagua uhai wa Chama.

Pia, Kinana aliagiza kuondolewa maofisa wote wa ushirika ambao hawana mashamba na wakulima wa Kahawa kuachwa kuuza Kahawa zao kwa bei wanazotaka kwa mtu yoyote.

“Uwezi kuwa kiongozi wa ushirika hauna Shamba kwa sababu hautaona maumivu ya wakulima, hivyo waondoeni.

“Amesema na kuongeza

“Wakati wa kulima hampo, wakati wa kuweka, dawa hampo, kwenye palizi hampo, kuvuna hatuwasaidii kuuza mpo hapa na kuwapangia namna ya kuuza, Kahawa yangu yako?” Amesema kwa kuhoji na kuongeza

“Nitakwenda kwa anayetoa pesa nzuri hata akitoka mbinguni, Mkuu wa Mkoa ( Albert Chalamila) simamia hili na tutakulinda, sio mtu ana kahawa yake analazimika kuuza kwa magendo.” Amesema

Kauli ya Kinana imekuja baada ya Mbunge wa Muleba Kusini, Dk Oscar Kikoyo kusema kuwa kuna ubabaishaji mkubwa katika uuzaji wa Kahawa.

“Mimi ni mwanasheria, najiuliza sipati jibu mpaka leo, mtu anatoa Kahawa kata moja kwenda kata nyingine anaambiwa ni magendo, sasa hiyo ni nini?”alihoji

Aidha, Kinana amesema vitendo vya kuwanyanyasa wakulima kunawafanya wauze kahawa zao kwa magendo kitu ambacho si sawa

“Kahawa ni yangu kwa nini niuze usiku na nipitishe kwa bodaboda? Ushirika liwepo kunyanyua watu au kunyonya watu?

“Nilikua Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, kuna siku nilikua na Rais Museven akaniambia kuna kiongozi mmoja alimfuata na kumwambia kuna wakulima wa kahawa walikua wanauza Kenya kwa hiyo azuie, Museven akamuliza kwa nini wanauza Kenya?yule kiongozi akajibu kwa sababu Kenya wananunua bei kubwa, aliwafokuza ofisini kwake, hawana kazi ya kufanya.

Hivyo nawaagiza muwaruhusu watu wauze kahawa zao wenyewe.

Habari Zifananazo

Back to top button